Jeremiah 13:22-26

22 aNawe kama ukijiuliza,
“Kwa nini haya yamenitokea?”
Ni kwa sababu ya dhambi zako nyingi
ndipo marinda yako yameraruliwa
na mwili wako umetendewa vibaya.
23Je, Mkushi aweza kubadili ngozi yake
au chui kubadili madoadoa yake?
Vivyo hivyo nawe huwezi kufanya mema
wewe uliyezoea kutenda mabaya.

24 b“Nitawatawanya kama makapi
yapeperushwayo na upepo wa jangwani.
25 cHii ndiyo kura yako,
fungu nililokuamuria,”
asema Bwana,
“kwa sababu umenisahau mimi
na kuamini miungu ya uongo.
26 dNitayafunua marinda yako mpaka juu ya uso wako
ili aibu yako ionekane:
Copyright information for SwhNEN